Free Web Hosting by Netfirms
Web Hosting by Netfirms | Free Domain Names by Netfirms


News
Habari



Neno litakuweka huru. Hii ni huduma ya NENO Evangelism MOMBASA "Haki za wanawake ni kubaki wanawake, wakati haki za wanaume ni kudumu wanaume. Wanawake hawawezi ya wanaume, pia wanaume hawawezi ya wanawake. Mashindano ya nini kati ya wanawake na wanaume? Kwa nini wanawake wanatamani kuwa wanaume?" Bado tuko katika ujenzi wa Web site hii. Habari zaidi baadaye



Huduma ya NENO
Kwenye Internet

http://nenosasa.netfirms.com

Tel. 254722410381 E-mail:
jamainga@yahoo.com
Huduma ya Neno sasa yatinga Nairobi
Mchungaji James Maina Ng'ang'a sasa ametua Nairobi. Kile alichokitamani siku nyingi sasa kimetimia. Mwenyewe anadai ni wakati wa Mungu umefika awe na huduma kubwa Nairobi, na hakuna mtu wala shetani atakayezuia hilo. Akizungumza kuhusu ajali mbaya aliyoipata karibuni, alisema amejua kwamba zilikuwa mbinu za shetani kumzuia asiingie Nairobi kwa kishindo. Kanisa lake liko barabara ya uhuru karibu kabisa na mahali lilipo kanisa la Redeemed ambalo linasimamiwa na Mchungaji Wilfred Lai. Sijui ilikuwaje, lakini hata Mombasa makanisa ya hawa wachungaji wawili huwa yamekaribiana kiasi cha kuwafanya watu waamini kwamba wanashindana. Lakini Ng'ang'a alisema kwamba yeye hashindani na Mtu bali anayeshindana naye ni Shetani. Kwamba imetokea kupata kiwanja jirani na kanisa jingine hiyo haina maana kwamba kuna ushindani wowote. Aliwahurumia wanaodhani kwamba yeye anashindana nao. Alisisitiza kwamba ni mawazo hayo potovu ndiyo yanayowafanya wengine wampige vita ambayo yeye hajajiandaa kupambana. Alimaliza kwa kusema wanajisumbua, na hawatafaulu kwani Mungu ameamua kumwandalia meza machoni pa watesi wake.


Serikali Kenya Darubini kwa Ng'ang'a

Kushoto ni Pastor James Maina Ng'ang'a, wakiwa na kiongozi wa kundi la MUNGIKI.
Mchungaji Maina Nganga alianzia Mombasa na sasa yuko Nairobi. Kanisa la Mombasa limefifia huku washirika wakihamia makanisa mengine. Aliyefaidi sana Mombasa ni mchungaji Panga ambaye washirika wengi wa Nganga wamehamia kwake. MTAKA YOTE HUKOSA YOTE ndivyo wanavyosema Mombasa. Wengine wanasema TAMAA ILIMPONZA FISI. Naye mchungaji Nganga anasema sasa Mungu amemwita Nairobi, na Mombasa ikae. Nayo serikali ya Kenya imekuwa ikimfuatilia kwa karibu mchungaji Ng'ang'a baada ya kiongozi wa kundi la Mungiki kudai ameokoka na kujiunga na kanisa la Ng'ang'a. Wanaiona hiyo kama mbinu ya MUNGIKI kuja na sura mpya ya kanisa la Neno Evangelism. Wengine wanamlaumu mchungaji Ng'ang'a kwa kujitakia makuu. Wengi wa washirika wake wanalalamika kwamba matumizi katika kanisa hilo ni ya juu kiasi kwamba hawawezi kuyamudu. Walitoa mfano wa vipindi katika redio na TV. Bei zake ni juu sana kwani kila wiki wanalazimika kulipa KSHS. 70,000 hiyo ni kwa ajili ya vipindi katika vyombo vya habari tu. Pia walisema kila mwezi hulazimika kulipia nyumba ya Mchungaji huko Nyali Mombasa na nyingine Runda Nairobi. Nyumba ya Mombasa ni KSHS 30,000 kila mwezi wakati ile ya Nairobi ni KSHS 40,000 kila mwezi. Walikumbusha kwamba nyumba hizo lazima zilipiwe miezi mitatu mbele. Tena walilalamika kuhusu michango ya kununua gari la mchungaji. Kwa imani mchungaji hupenda kuendesha gari kubwa ya kifahari na ya kisasa kabisa. Kwa sababu kampuni za magari hutoa magari kila kukicha, hakuna siku watamaliza kununua gari la mchungaji. Likitoka jipya mchungaji anasema ataliendesha kwa imani. Imani ya mchungaji inawalazimu washirika waingie mifukoni kuitimiza imani hiyo. Wengi waliokuwa wakuu katika mashirika imewabidi wafutwe kazi baada ya mashirika hayo kupata hasara ya mamilioni ya pesa. Kuna wale wanaosema hasara kwenye mashirika hayo ilisababishwa na ufujaji wa pesa zilizopelekwa kanisani kulipia gharama za juu kanisani ambazo hakuna dalili kwamba zitamalizika karibuni. Ni kweli kila mtu amepewa huduma tofauti na mwingine, lakini tofauti hiyo ikiwa ni kuwalemea washirika na mahitaji ya pesa yasiyoisha, tuna mashaka kama na hiyo ni huduma ya Mungu.


Siyo kweli kwamba wahubiri ni watu waliokosa la kufanya.
Mchungaji James Maina Nganga alikuwa na mengi ya kufanya kabla hajaanza kuhubiri. Alipotoka jela alianza kuuza kaseti za nyimbo za injili akitumia baiskeli.


Mchungaji James Maina Nganga, tayari kikazi.


Pasror Mr. and Mrs. James Maina Nganga
"Haki za wanawake ni kubaki wanawake, wakati haki za wanaume ni kudumu wanaume. Wanawake hawawezi ya wanaume, pia wanaume hawawezi ya wanawake. Mashindano ya nini kati ya wanawake na wanaume? Kwa nini wanawake wanatamani kuwa wanaume?"




Pastor James Maina N'gan'ga.
"UPAKO huleta mali, lakini mali haiwezi kuleta UPAKO." Utafuteni kwanza ufalme wa Mungu na haki yake na hayo mengine mtazidishiwa.


Mchungaji Maina akiwa na gari yake ya kifahari kabla haijapata ajali.


Huwezi kuamini baada ya ajali hii mbaya Mchungaji Ng'ang'a alitoka bila majeraha yeyote. huo ni muujiza wa Mungu kwa mtumishi wake. Mwenyewe amekuwa akihubiri kwamba hatawahi pata ajali maishani mwake. Pengine ajali hii ni fundisho kwake na kwetu pia. Mungu asifiwe. Kwa sasa Kanisa la NENO Nairobi linakita mizizi jambo linalozua upinzani mkubwa kutoka hata kwa wachungaji marafiki zake. Kitonga aliyekuwa rafiki wa karibu, sasa i8nasemekana ndiye anayepinga kwa nguvu zote kanisa la NENO kujengwa karibu na NGOME yake Nairobi.




Tangaza Biashara yako Bure
Tuma picha na maelezo kwa munishifaustin@yahoo.com

http://munishi.com
Send a photo and information to munishifaustin@yahoo.com

Neno litakuweka huru Msikilize mchumngaji James Maina Nganga kila Jumamosi saa tatu asubuhi katika KBC TV "Haki za wanawake ni kubaki wanawake, wakati haki za wanaume ni kudumu wanaume. Wanawake hawawezi ya wanaume, pia wanaume hawawezi ya wanawake. Mashindano ya nini kati ya wanawake na wanaume? Kwa nini wanawake wanatamani kuwa wanaume?"Bado tuko katika ujenzi wa Web site hii. Habari zaidi baadaye

 


Study The Bible

Passage (eg. John 3:16):

Search word(s) (eg. saved):


Pastor james Maina Nganga Tell. 254722410381 Mombasa Kenya East Africa
E-mail:
E-mail: jamainga@yahoo.com

Check mail at Hotmail

Check Mail at Yahoo